Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 20:59

Nigeria na Somalia waelezea khofu ya ukaguzi Marekani


Raia wa Nigeria na Somalia wameelezea khofu zao kufuatia hatua mpya ya ukaguzi na masharti kwa wasafiri wa ndege, zilizochukuliwa na serikali ya Marekani duniani kote. Sheria hizo mpya za Marekani zimewekwa kwa raia kutoka nchi 14 ikiwemo Nigeria, Somalia na Sudan.

Mabadiliko hayo na ukaguzi huo mkali unafuatia tukio la siku ya Krismas, ambapo raia mmoja wa Nigeria alijaribu kulipua ndege moja ya Marekani katika mji wa Detroit.

Wasafiri kutoka Lagos huko Nigeria walitakiwa kuwasili kwenye viwanja vya ndege zaidi ya saa saba, kabla ya kuondoka kuelekea Atlanta, Georgia. Jimbo la kusini hapa Marekani na kusababisha mlolongo mrefu wa wasafiri.
Pia wasafiri kutoka Somalia wamewekewa masharti makali ya ukaguzi ambayo pia yamewabughudhi wasomali walio wengi katika jimbo la Minnesota hapa Marekani.

Nchi zingine zilizowekewa masharti kama hayo ni abiria kutoka Sudan, Cuba, Iran, Syria, Afghanistan. Mataifa mengine ni Algeria, Irak, Lebanon, Libya, Pakistan, Saudi Arabia na Yemen.

XS
SM
MD
LG