Kundi la waasi la al-Shabab nchini Somalia, linasema litapeleka wapiganaji Yemen kuwasaidia wanamgambo wa Al-Qaida.
Afisa mmoja wa cheo cha wa al-Shabab alisema leo Ijumaa kwamba kundi litakwenda kuwasaidia wanamgambo, ambao wanapigana na majeshi ya serikali ya Yemen. Afisa huyo Sheikh Mukhtar Robow Abu Mansour, alitoa wito kwa wa-Islam katika nchi nyingine kujiunga kwenye mapambano hayo.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari pia alionesha mamia ya wapiganaji wapya wa al-Shabab waliopewa mafunzo wakishangilia na kusema Allahu Akbar au mungu ni mkubwa.
Serikali ya Yemen imezuia mfululizo ya mashambulizi na mapigano ya anga dhidi ya kundi la al-Qaida lililopo eneo hilo, lijulikanalo kama Al-Qaida katika Peninsula ya Arabuni. Walisema shambulizi moja la anga wiki iliyopita katika jimbo la mashariki mwa Shabwa, liliuwa washukiwa wanamgambo 34.