Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 00:30

Kenya yatakiwa kuchukua hatua kali dhidi ya walanguzi wa mihadarati


Makundi ya kijamii nchini Kenya yameitaka serikali nchini humo iwachukulie hatua kali walanguzi wa madawa ya kulevya ambao wamezorotesha juhudi za kupambana na matumizi ya madawa hayo.

Makundi hayo yamesema matamshi ya Rais Mwai Kibaki kuwa matumizi ya madawa hayo yameathiri maisha ya vijana wengi haitoshi kwani walanguzi huingiza madawa hayo nchini kupitia mipaka inayolindwa na maafisa wa serikali.

Wamesema wakenya wamechoka kuwaona vijana wakiendelea kutumia madawa ya kulevya licha ya kampeni zinazoendelezwa za kupambana na matumizi ya madawa hayo yanayoingia nchini humo kutoka Afghanistan na Pakistan kupitia bahari ya Hindi.

Viongozi wa makundi hayo wanashikilia kuwa juhudi zao zimegonga mwamba kwani madawa hayo yanaendelea kuingia nchini humo kama kawaida.

Rais wa Kenya Mwai Kibaki ambaye yupo kwenye ziara katika mkoa wa pwani nchini humo alisema kwamba suala la matumizi ya madawa ya kulevya linatisha kwa kizazi cha vijana ambao sasa hawajui waendako. Licha ya matamshi hayo ya Rais Kibaki, viongozi hao wa makundi ya jamii wanasisitiza kuwa serikali ya Kenya ina uwezo wa kupambana na suala la madawa ya kulevya nchini humo.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG