Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 28, 2022 Local time: 22:49

Wasi wasi Kuhusu Usalama Kenya


Hali ya taharuki imeanza kutanda katika maeneo mbali mbali ya jimbo la Rift Valley nchini Kenya, baada ya polisi kugundua makaratasi ya uchochezi yanayotawanywa dhidi ya jamii fulani katika eneo hilo. Makaratasi hayo yanaionya jamii ya kabila la Wajaluo kuondoka katika jimbo la Rift Valley kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

Hii si mara ya kwanza kwa makaratasi ya aina hii kutawanywa katika jimbo la Rift Valley, na makundi ya watu wasiojulikana. Kitendo kama hiki kilishatokea kabla na baada ya uchaguzi mkuu ambapo watu wasiojulikana walifanya hivyo, kutokana na misimamo ya kisiasa dhidi ya viongozi wa eneo hilo.

Taharuki hii kati ya jamii ya kabila la Wakalenjin anakotoka Waziri wa kilimo, William Ruto, pamoja na jamii ya Wajaluo anakotoka Waziri Mkuu Raila Odinga, imesababishwa na mvutano katika mgogoro wa msitu wa Mau, ambapo Waziri Mkuu anasisitiza jamii ya Wakalenjin waliovamia msitu huo wakati wa utawala wa Rais wa zamani Daniel Arap Moi, waondolewe.

Badala ya kuwepo na maafikiano kati ya mawaziri na jamii zote nchini Kenya kuhusu umuhimu wa msitu huo wa Mau, suala hili sasa limegeuka na kuchukua sura mpya ya kisiasa. Waziri wa kilimo nchini humo, William Ruto, anadai kwamba Waziri Mkuu Raila Odinga anajitafutia umaarufu kupitia msitu wa Mau.

XS
SM
MD
LG