Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 12:58

Obama: viongozi duniani wakubali mkataba


Rais wa Marekani Barack Obama amewaambia viongozi wa dunia leo Ijumaa, katika siku ya mwisho ya mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa huko Copenhagen, kwamba wakati umefika kwa mataifa duniani kuungana pamoja kutafuta suluhisho.

Washiriki wameshindwa baada ya mazungumzo ya wiki mbili kupata mkataba wa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu, ambapo wanasayansi wengi wanalalamikia hali ya joto joto duniani.

Vyombo vya habari vinasema maandishi ya rasimu ya mkataba, ambao unaweza kubadilika, hauelezei kwa kina njia zinazolenga kukata gesi chafu katika mataifa yenye viwanda vikubwa duniani, na kutofikia lengo la kupata mkataba utakaokuwa sheria.

Akikubaliana na hilo kwamba baadhi ya mataifa yanahisi Marekani haijishughulishi vya kutosha, bwana Obama alisema viongozi wa dunia lazima wakubali mkataba huo, hata kama una mapungufu.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon aliwasihi washiriki wa mkutano leo Ijumaa kusonga mbele kupata suluhisho, lenye kufaa na kupeana matumaini.

XS
SM
MD
LG