Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:11

Makubaliano yafikiwa juu ya kura ya maoni Sudan


Makubaliano ya mswada wa sheria yaliyofikiwa kati ya vyama vikuu vya Sudan Kaskazini na kusini yatawasilishwa bungeni Jumatatu kuidhinishwa kua sheria kabla ya kura ya maoni ya 2011.

Viongozi wa chama cha kaskazini cha National Congress Party-NCP cha Rais Omar al-Bashir na Sudan People's Liberation Movement-SPLM, cha eneo la kusini, wanasema wamekubaliana juu ya miswada mitatu ya sheria juu ya kura ya maoni ya kuwauliza wakazi wa kusini ikiwa wanataka uhuru wao au kubaki pamoja na eneo la kaskazini kama nchi moja

Sheria ya pili ni kuwauliza wakazi wa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Abyei ikiwa wanataka kujiunga na eneo la kusini. Na sheria ya tatu iliyokubaliwa Jumapili nikushauriana na wakazi juu ya mustakbali wa jimbo la Blue Nile lililopo kusini.

Tatizo kubwa la kura ya maoni lilikua juu ya uwamuzi wa matokeo ya kura ya maoni. Chama cha NCP kilitaka ushindi wa theluthi mbili za kura, wakati SPLM walitaka uwamuzi wa zaidi ya asilimia 50 kua ni ushindi.

Makubaliano yanamaliza mivutano ya miezi kadhaa kati ya SPLM na NCP, baada ya wajumbe watatu wakuu wa SPLM kukamatwa kwa muda na kuachiwa Jumatatu iliyopita kufuatia malalamiko ya kutaka mageuzi ya kidemokrasia mbele ya bunge la Sudan.




XS
SM
MD
LG