Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 01:20

Waziri Clinton ampeleka Gration Sudan


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton, anampeleka mwanadiplomasia mmoja wa cheo cha juu nchini Sudan katika juhudi za kutuliza ongezeko la mivutano kabla ya uchaguzi wa mwezi April.

Waziri Clinton alitangaza jana Alhamisi, kwamba mwakilishi maalumu kwa Sudan, Scott Gration, atarudi katika nchi hiyo ya Afrika wiki hii. Hatua hiyo imekuja baada ya polisi wa Sudan kupigana na waandamanaji kutoka vyama vya upinzani, na eneo lililojitenga la Sudan kusini, nje ya bunge huko Khartoum siku ya Jumatatu.

Kundi la haki za binadamu la Amnesty International, linasema polisi waliwakamata zaidi ya watu 200 na waliwatesa baadhi yao wakiwa kizuizini. Clinton alilaani ukamataji huo, akisema uhuru wa kukutana na kuzungumza ni muhimu sana kwa uchaguzi wa kuaminika. Alisema pia waandamanaji hawatakiwi kuwa na khofu, kuwa huenda watakamatwa au kuwekwa kizuizini.

Waziri Clinton alisema Gration atasaidia kuanza tena kwa majadiliano ili kuvisaidia vyama hasimu nchini Sudan kumaliza tofauti zao kwa amani.

XS
SM
MD
LG