Katika sherehe zilizofanyika chini ya ulinzi mkali kabisa kuwahi kutokea huko Norway, Obama alipokea rasmi tuzo yake, akifahamu utata uliyopo kuhusu kuteuliwa kwake kamati ya Nobel. Na moja kwa moja aliwajibu walokosoa uwamuzi huo akisema, "kwa sehemu ninafahamu, ndiyo mwanzo ninanaza na wala sio mwisho wa kazi zangu kwenye jukwa la kimataifa."
Lakini alisema suala kuu linalosababisha utata huo ni kwa sababu yeye ni kiongozi wa taifa linalokabiliana na vita viwili. Kwa hivyo anasema anamefika huko akifahamu fika gharama za vita, kukiwepo na masuala magumu chungu nzima kuhusu uhusaino kati ya vita na amani na juhudi zao za kubadilisha moja kwa ajili ya nyengine.
Rais Obama akikabiliwa ba changamoto hiyo alijaribu kufafanua juu ya vita vya haki na amani ya kudumu. Alisema kwanza inabidi kukiri ukweli kwamba hatutoweza kukomesha ugomvi wote wa kutumia nguvu wakati wa uhai wetu. alisema, "kuna wakati pale mataifa yakichukua hatua binafsi au kushirikiana na wengine watagundua utumiaji wa nguvu si jambo muhimu tu bali linakubalika."
Kamati ya Nobel ilipotangaza uwamuzi wake wa mshindi wa Amani mwaka 2009, ilitaja juhudi za rais Obama kuimarisha diplomasia ya kimataifa na ushirikiano. Ilieleza aliweza kuleta muamko mkubwa duniani kutokana na ujumbe wake wa matumaini.
Uchunguzi wa maoni hapa Marekani unaonesha wa Marekani wanamini heshma alipewa mapema mno. Na nje ya tasisi ya Nobel, kundi la wakazi wa Norway alikua wakieleza maoni hayo hayo wakimba "Obama umeshaipata sasa ifanyiye kazi."