Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:43

Tanzania, Zitto hakiachi Chadema


Naibu Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, Chadema, Zitto Kabwe Zubeiri anasema, licha ya hali ya kutoelewana ndani ya chama chake, hatojiondoa na kwamba hizo ni hisia tu za watu.

Akizungumza na Sauti ya Amerika, Zitto amesema "kwa sababu watu wamezoea kwamba watu wakigombana, wasipoelewana ndani ya vyama, basi ni lazima mtu atoke ajiunge na chama kingine. Kwa hiyo Siondoki Chadema na ninaendelea kua mwanachama wa Chadema."

Mbunge huyo alisema ni jambo la kawaida kwa watu kutoelewana na kwamba kuna tofauti ya mitizamo ndani ya chama. Anasema kuna tofauti za mitizamo kuhusiana na suala la demokrasia ndani ya chama,kuhusu uwajibikaji ndani ya chama, kuna suala la kuheshimiana ndani ya chama lakini siyo tofauti za kumwezesha kukihama chama hicho.

Zitto anasema "sikujiunga mimi na Chadema labda kwa sababu nilikwenda kwenye kura za maoni za chama kingine nikakataliwa ndipo nikapata hasira na nikajiunga na Chadema, hapana. Nilijiunga na Chadema kutokana na kuamini misingi ya Chadema, walakini ni wazi kabisa kwamba ni lazima ifikiye wakati viongozi inapokua hamuelewani, ni lazima moja apishe nagfasi ya wengine watekeleze majukumu yao."

Amesema ikiwa ataondoka, basi ataondoka kakutoka uwongozi lakini si uwanachama. Na anasema hamini nadharia ya kuhama chama, kama vile alivyo pinga kuhama kwa Thomas Kashilila na kujiunga na NCCR Mageuzi.

XS
SM
MD
LG