Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 01:17

Wajumbe wataka mkataba wa haraka wa hali ya hewa


Akiufungua mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Hali ya Hewa, huko Copenhagen siku ya Jumatatu mwenyeji waziri mkuu wa Denmark Lars Lokke Rasmussen aliwambia wajumbe kwamba kishinikizo kinaongezeka cha kupatikana mkataba wa kimataifa kuchukua nafasi ya mkataba wa Kyoto unaomalizika 2012.

Alisema zaidi ya viongozi kutoka mataifa 100 pamoja na rais wa Marekani Barack Obama watahudhuria siku za mwisho wa mkutano huo wa siku 12.

Mkuu wa jopo la Umoja wa Mataifa la wanasayansi wa hali ya hewa, Rajendra Pachaurai alisema kuna hitajika hatua ya kimataifa kupunguza matukiyo ya vimbunga joto kali mafuriko ya maeneo ya pwani na ukame.

Mkua wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa Yvo de Boer akikihutubia kikao cha ufunguzi alisema. "wakati umefika wa kutekeleza," baada ya miaka miwili ya mazungumzo ya kufikia mkataba utakaochukua nafasi ya mkataba wa Kyoto.

Wajumbe wa majadiliano kabla ya mkutano wa viongozi wamedokeza kutokea mgawiko kati ya mataifa tajiri na mataifa yanyoendelea juu ya kiwango cha kupunguza uzalishaji wa gesi za sumu na kiwango cha msaada unaohitajika kusaidia mataifa maskini.

XS
SM
MD
LG