Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 12:06

Uchaguzi unafanyika kwa amani huko Comoros


Duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge na mabaraza ya visiwa ulifanyika kwa amani huko visiwani Komoro, ingawa upinzani unadai kumekuwepo na vitisho dhidi ya wafuasi wa upinzani.

Mwandishi wa sauti ya Amerika huko Moroni anasema baada ya kuchelewa kufunguliwa vituo kwa masaa mawili asubuhi, wapigaji kura walijitokeza kwa wingi wakati wa alasiri na kusababisha msongamano katika vituo vingi vya kupiga kura.

Wagombea wa mungano wa Rais Ahmed Abdallah Sambi, wameendesha kampeni kwa msingi kwamba kumekuwepo na utulivu wa kisiasa chini ya utawala wake hasa baada kumondowa kiongozi wa waasi kutoka kisiwa cha Nzawni 2008.

Upinzani umeituhumu serekali ya Rais Sambi kwa kuwabughudhi wagombea wao na wafuasi wao wakati wa kampeni za wiki mbili. Ushindi wa upinzani utapelekea kuwepo na mvutano mkubwa kwa bunge kuidhinisha mabadiliko ya katiba.

Kwani jukumu kuu la kwanza la wabunge litakua kuidhinisha matokeo ya kura ya maoni ya mapema mwaka huu kufanya mabadiliko ya katiba pamoja na kuidhinisha kuongeza muda wa mhula wa rais Sambi kwa miaka miwili.

Kulikuwepo na zaidi ya wagombea 300 kugombania viti 24 vya bunge na viti vya mabaraza ya visiwa. Duru ya pili ya uchaguzi wa wagombea amabo hawakupata zaidi ya asilki mia 50 itafanyika baada ya wiki mbili.

XS
SM
MD
LG