Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 18:01

Hali ya Kapteni Camara yatia wasi wasiKiongozi wa kijeshi Kapteni Moussa Dadis Camara, inasemekana yupo katika hali mbaya huko Morocco, tofauti na ilivyoripotiwa awali.

Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa, Rais wa Burkina Faso, Blaise Compaore, aliielezea hali ya Kapteni Camara kama mbaya, lakini si ya wasi wasi. Alisema anafikiri kiongozi huyo wa Guinea atafanyiwa upasuaji kwa sababu alipigwa risasi kichwani, katika jaribio la mauaji siku ya Alhamisi.

Bwana Campaore ni mpatanishi wa eneo katika matatizo ya kisiasa nchini Guinea. Alisema taarifa zimekuja kutoka kwa daktari binafsi wa kiongozi huyo wa Guinea.

Waziri wa habari wa Guinea alisema awali kwamba Kapteni Camara alipata majeraha kidogo na aliweza kutembea na kuzungumza kama kawaida. Alisema Camara mwenye umri wa miaka 45 alipata jeraha la risasi kichwani. Waziri huyo wa habari alimtaja mpambe wa karibu wa Rais, Aboubacar Toumba Diakite, kuwa anahusika na shambulizi.

Maafisa wa jeshi baadae walisema Diakite alikamatwa. Diakite anashutumiwa kuongoza majeshi ya usalama yaliyofyatua risasi kwenye maandamano ya upinzani mjini Conakry mwezi September. Mauaji hayo yamepelekea mzozo wa kisiasa nchini humo.

Makundi ya haki za binadamu yanasema wanajeshi wa Guinea waliwauwa zaidi ya waandamanaji 150 waliokusanyika kwenye uwanja wa mpira, huku serikali inasema chini ya watu 60 waliuwawa.

XS
SM
MD
LG