Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 13:15

Siku ya Ukimwi Duniani


Dunia imeadhimisha siku ya ukimwi Disemba mosi kwa kutoa mwito wa kila mathiriwa kupata matibabu na kuimarisha haki za binadam. Umoja wa Mataifa unasema kumekuwepo na maendeleo makubwa katika watu kupata huduma, huku idadi ya watu wepya wanaoambukizwa na virusi vya HIV inapunguka na watoto wachache wanazaliwa wakiwa wameambukizwa na HIV.

Hata hivyo ripoti ianeleza kwamba idadi ya watu wenye HIV inazidi kuongezeka nakuna watu milioni 4 hivi sasa wanapata matibabu kati ya watu milioni 33 wanaoishi na HIV na Ukimwi.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anasema nchi yake itaongeza huduma za upimaji ugonjwa wa ukimwi na huduma ya dawa kwa wagonjwa.

Bwana Zuma alitangaza juhudi hizo siku ya Jumanne kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani, huko Afrika kusini, ambapo taifa hilo limeathiriwa vibaya na virusi vya HIV/ukimwi. Alisema ifikapo mwezi April mwakani, nchi hiyo itatoa huduma kwa watoto wote walio chini ya mwaka mmoja, ambao wamepimwa na kukutwa na virusi vya HIV, ambavyo vinasababisha ugonjwa wa ukimwi.

Bwana Zuma pia alitaka kumalizika kwa ubaguzi dhidi ya waathirika wa HIV. Ujumbe kama huo ulisemwa Jumanne kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon. Katika taarifa yake, bwana Ban alizisihi nchi kuondoa sheria na sera ambazo zinawaumiza waathirika wa ukimwi, ikiwemo marufuku ya kusafiri kwa watu walioambukizwa virusi vya HIV.

Jumatatu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton alisema utawala wa Obama utaondoa marufuku ya muda mrefu kwa wageni wenye HIV kuingia Marekani, mwanzoni mwa mwaka ujao na kwamba Washington itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa ukimwi mwaka 2012.

XS
SM
MD
LG