Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 07:27

Interpol yakamata pembe za ndovu


Maafisa barani Afrika wamekamata zaidi ya kilo elfu moja ya pembe haramu za ndovu, na kufanya ukamataji kadhaa katika uchunguzi wa mataifa mbali mbali juu ya uwindaji haramu na magendo.

Shirika la kimataifa la polisi-Interpol, lilisema jana Jumatatu uchunguzi uliwahusisha maafisa kutoka nchi sita za Kenya, Burundi, Ethiopia, Rwanda,Tanzania, na Uganda. Shirika hilo lilisema ukamataji huo wa pembe za ndovu ni mkubwa kuwahi kutokea.

Interpol ilisema maafisa katika nchi zote sita walifanya ukaguzi na kuvamia maduka na masoko. Maafisa pia walipekua magari katika vituo vya ukaguzi mipakani. Kwa kuongezea biashara haramu ya pembe za ndovu, Interpol ilisema uchunguzi huo uligundua ngozi za chui, na silaha.


XS
SM
MD
LG