Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 17:12

Marekani na India kuimarisha ushirikiano wao


Rais Barack Obama wa Marekani na waziri mkuu wa India wameahidi kufanya kazi pamoja kuimarisha uchumi wa dunia, kupunguza mabadiliko ya hali ya hewa, kupunguza kuenea kwa silaha za nuklia pamoja na kupambana na ugaidi.

Viongozi hao wawili walisisitiza haja ya utulivu wa kisiasa huko Asia ya Kusini. Bw Obama alisema si jukumu la Marekani kuzieleza India na Pakistan namna ya kuendeleza uhusiano wao, lakini alisema anamatumaini kwamba hatimae pakistan inakabiliana na makundi ya kigaidi yanayoendesha shuhguli zake katika ardhi yake.

Rais Obama na mgeni wake waziri mkuu wa India Singh walizungumza Jumanne mchana na waandishi wa habari baada ya kukutana kwa mazungumzo juu ya uhusiano kati ya nchi zao mbili pamoja na masuala mengine ya kimataifa.

Usiku wa Jumanne Rais Obama alimuandalia waziri mkuu wa India na mkewe dhifa ya kitafia, ya kwanza kufanywa na utawala wake. Rais Obama alikubali mualiko wa kuitembelea India mwakani na familia yake.

Nchi hizi mbili zilianzisha ushirikiano mpya wa kiuchumi, na waziri wa fedha wa Marekani Timothy Geithner anatazamiwa kusafiri hadi India mwakani kuzindua tume itakayo imarisha ushirikiano wao.

XS
SM
MD
LG