Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 23:08

Rais wa Nigeria kwenda Saudi Arabia kwa matibabu


Rais wa Nigeria Umaru Yar’Adua anakwenda Sudi Arabia jumatatu kwa ajili ya iuchunguzi wa afya yake.

Ofisi ya rais imesema bwana Yar’Adua anatarajiwa kumpigia simu daktari wake binafsi katika mji wa Jeddah kwa ajili ya kufuatilia afya yake.

Bwana Yar’Dua ana ugonjwa sugu wa figo na amewahi kwenda Ujerumani na Saudi Arabia mara nyingi miaka mitatu iliyopita kwa ajili ya matibabu kiafya.

Wakosoaji wameuliza kama rais huyo mwenye umri wa miaka 58 yuko sawa kiafya kuongoza taifa hilo maarufu katika bara la Afrika.

Hii itakuwa mara ya tatu kwenda Saudi Arabia tangu mwezi Augosti.

XS
SM
MD
LG