Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:31

EAC yakubaliana juu ya soko la pamoja


Marais wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki wanaokutana Arusha,Tanzania kuadhimisha miaka 10 ya umoja huo wametia saini mkataba wa soko la pamoja la nchi hizo na kuzindua mradi wa kutoa kompyuta za bure za mkononi - Laptop - kwa shule za msingi kutoka nchi wanachama wa jumuia hiyo. Mara baada ya mkataba huo kutiwa saini viongozi wa taasisi na wakuu mbali mbali wa biashara nchini Tanzania, wametoa maoni mbali mbali kuhusu faida ya soko la pamoja.

\Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Tanzania, Sirel Chami, aliwataka wa-Tanzania kuongeza ubora wa bidhaa zao wanazozalisha ili kukidhi haja ya soko hilo la pamoja.

Amesema “kama una kiwanda chako na unaajiri watu 500, sasa unaweza ukaajiri watu elfu mbili” kwa hiyo unaweza ukajenga ajira zaidi kwa wa-Tanzania kwa sababu soko limepanuka. Vile vile unachangia zaidi katika pato la Taifa kwa sababu utalipa kodi kubwa zaidi na unapolipa kodi kubwa zaidi inamaanisha kwamba Taifa litakuwa na uwezo zaidi wa kuboresha huduma za barabara, shule, maji na sekta nyingine ambazo zinahitajika nchini humo.

Kwa upande wa sekta binafsi serikali ya Tanzania inasema imeshaanza kuwaandaa wafanyabiashara wa Tanzania ili kuweza kumudu ushindani katika taratibu mpya za soko la pamoja katika nchi tano husika za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG