Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 02:00

Hatari ya gesi katika Ziwa Kivu


Hali imekuwa ya wasi wasi miongoni mwa raia huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, tangu itolewe ripoti kuhusu uwezekano wa kutokea mlipuko wa gesi ya Carbon Dioxide na ile ya Methane kwenye ghuba ya Kaguno katika jimbo la Kivu kaskazini nchini humo.

Kwa wakati huu serikali ya Congo haina uwezo wa kuzuia gesi hiyo na inaendelea kusubiri msaada kutoka Benki Kuu ya Dunia ambayo iliahidi kutoa Euro milioni tatu.

Mtafiti Michel Albwch, Profesa kutoka chuo kikuu cha Sazoie nchini Ufaransa ambaye aliongoza timu ya wataalamu na watafiti wa masuala ya Volcano na majanga asilia amesema kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kutokea mlipuko wa gesi ya Carbon Dioxide kwenye ziwa Kivu kwenye mpaka wa DRC na Rwanda, ikiwa hakutakuwepo juhudi za kuondoa gesi hiyo haraka iwezekanavyo.

Mtafiti huyo amesema kuna uwezekano wa kuondolewa gesi hiyo ndani ya ziwa Kivu na ni jambo la kufurahisha kwa sababu haitokea kila mara kugundua tatizo kabla ya janga kutokea. Lakini hata hivyo Profesa Albwch ametoa wito kwa raia waendelee kuwa watulivu.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG