Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 14:59

Rais Obama awasili China kuimarisha uhusiano


Rais wa Marekani Barack Obama aliwasili Shangai Jumapili usiku ambako atakua na mazungumzo na wakuu wa mji na wanafunzi wa chuo kikuu siku Jumatatu. Ataelekea Bejing baadae kwa mazungumzo na viongozi wa serekali ya China hadi siku ya Jumatano.

Waziri wa mambo ya nchi za nje Hillary Clinton alieleza uhusiano kati ya Washington na Bejing kua ni mzuri, alipokua anazungumza na kipindi cha televisheni "Meet the Press" cha kituo cha NBC siku ya Jumapili. Alisema tayari kumekuwepo na matokeo mazuri kutokana na Bejing kukubaliana na vikwazo vya kimataifa dhidi ya Korea ya kaskazini na kuunga mkono juhudi za kuwasilianana Iran kuhusiana na mpango wake wa nuklia.

Maafisa wa White House wamesema Rais atakua na mazungumzo na wanafunzi juu ya ushirikiano kati ya Marekani na China wakati wa mkutano ndani ya ukumbi huko Shanghai. Atajibu masuali ya wanafunzi watakaohudhuria pamoja na masuali ya watu walouliza kupitia tovuti.

Rais wa Marekani amesema Washington inajaribu kuimarisha zaidi ushirikiano wake na Bejing na wala si kuidhibiti taifa hilo kuu la Asia.

XS
SM
MD
LG