Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:50

Mafuriko yaongezeka Tanzania


Mvua kubwa zilizonyesha siku tofauti katika maeneo mbali mbali nchini Tanzania zimesababisha maafa makubwa yakiwemo vifo na uharibifu wa nyumba.

Maeneo mengine ambayo yamekumbwa na mafuriko kwa nyakati tofauti, mbali na mkoa wa Kilimanjaro na kusababisha maafa nchini Tanzania ni pamoja na mikoa ya Dodoma, Morogoro, Kigoma na Iringa. Mvua kubwa zilizonyesha mkoani Dodoma Alhamisi usiku zilisababisha zaidi ya magari 300 kukwama baada ya maji kujaa katika daraja lililopo eneo la Kibaigwa.

Wakati huo huo Mkoani Kigoma watu walikoseshwa makazi baada ya mvua kubwa kunyesha ikiambatana na upepo mkali na kuezua mapaa ya nyumba.

Mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania Filbert Tibaijuka akikaririwa na vyombo vya habari alisema kuwa mvua hizo zinazonyesha katika sehemu mbali mbali nchini si za El nino. Mamlaka ya hali ya hewa imesema mvua hizo bado ni za kawaida na hazijafikia kiwango cha kuitwa hicho cha El nino, licha ya kutoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini na mvua hizo. Mamlaka hiyo pia imetahadharisha kuwa kuna baadhi ya maeneo ambayo yataendelea kukosa mvua na hivyo kuwataka wananchi kupanda mazao yanayostahmili ukame.

XS
SM
MD
LG