Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 23:37

Habari kuu za wiki Tanzania na Rwanda


Wiki hii Tanzania ilikumbwa na mvua kubwa zilizosababisha maafa na zaidi ya watu 20 kupoteza maisha yao. Akizungumza na sauti ya Amerika katika meza ya waandishi habari, mwandishi habari Musa Juma wa gazeti la ‘Mwananchi’ mjini Arusha, alisema juhudi zilikuwa bado zinaendelea kutafuta maiti au watu walionusurika maporomoko ya tope katika wilaya ya Same mkoa wa Kilimanjaro.

Bwana Juma pia alielezea juu ya mkutano unaoendelea mjini Arusha wa wabunge wa jumuiya ya Afrika Mashariki ambao unaandaa mkutano mkubwa wa marais wa nchi tano za jumuiya hiyo utakaofanyika Novemba 20 . Jumuiya itazungumzia mustakabal wa kuelekea katika shirikisho la nchi tano hizo.

Akishiriki katika mazungumzo hayo mwandishi habari Flora Kaitesi wa Radio Rwanda, alielezea juu ya mkutano wa tano wa kitaifa uliozungumzia manyanyaso ya watoto. Bi Kaitesi alisema watoto waliomba rais Paul Kagame kusaidia katika utekelezwaji kamili wa maazimio yaliyofikiwa katika vikao vya awali, yatakayowasaidia watoto kupambana na manyanyaso dhidi yao.

Bi Kaitesi pia alielezea juu ya mkutano uliofanywa Kigali na kuhudhuriwa na waendesha mashitaka wakuu wa mahakama za kimataifa za uhalifu wa kivita akiwemo Luis Moreno Ocampo wa mahakama ya ICC.

XS
SM
MD
LG