Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 19:33

Mapendekezo ya Katiba mpya Kenya kuchapishwa karibuni


Jopo la wataalamu nchini Kenya wanaotathimini marekebisho ya katiba nchini humo, tayari wameandika kielelezo ambacho kinatarajiwa kuchapishwa na baadaye kujadiliwa katika juhudi za kuandaa katiba mpya ya Kenya. Mapendekezo hayo ni pamoja na kupunguzwa kwa madaraka ya rais, kuwepo kwa waziri mkuu mwenye madaraka ya kiutendaji na bunge lenye mabaraza mawili.

Wataalam wa maswala ya katiba na wachambuzi wa habari wanasema hiyo ni hatua kubwa katika juhudi za kuipatia Kenya katiba mpya, lakini wanatahadharisha kwamba bado kuna kazi kubwa ya kufanywa kufanikisha zoezi hilo. Sauti ya Amerika imezungumza na wakili wa masuala ya sheria P.L.O Lumumba na kumuuliza mapendekezo yaliyomo katika kielelezo hicho.

XS
SM
MD
LG