Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 27, 2023 Local time: 13:57

Jenerali Kazini wa Uganda auawa na mpenzi wake


Vyanzo vya habari nchini Uganda vinasema Mkuu wa majeshi wa zamani nchini humo, Meja Jenerali Kazini, ameuawa ndani ya flati ya mpenzi wake mjini Kampala. Ripoti zinasema alipigwa kichwani na gongo la chuma wakati wa ugomvi na mpenzi wake wa kike. Msemaji wa jeshi alisema Kazini alikuwa muathirika katika mzozo ndani ya nyumba. Mpenzi wake wa kike amekamatwa.

Meja Jenerali Kazini aliondolewa kama mkuu wa jeshi mwaka 2003 baada ya Umoja wa Mataifa kumshutumu kwamba alichukua rasilimali huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wakati akiongoza oparesheni za jeshi la Uganda nchini humo.

Alikuwa anasimamia majeshi ya Uganda ambayo yalipigana na wenzao wa Rwanda huko Mashariki mwa DRC katika mji wa Kisangani mwaka 1999. Taarifa zaidi zinasema watu wengi wameshtushwa na mwenendo wa kifo chake.

Mwaka jana Meja Jenerali Kazini alikutwa na shutuma za rushwa, madai ambayo hayana uhusiano na shutuma za Congo. Aliwekwa jela, lakini alitolewa kwa dhamana na alikuwa anakabiliwa na mashtaka kukaidi amri.

XS
SM
MD
LG