Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:29

Maharamia wa Somalia washambulia Meli Bahari ya Mbali


Maharamia wa ki-Somali wamefanya shambulizi dhidi ya meli ya mafuta kilomita 1,850 kwenye mwambao wa Somalia – umbali mkubwa kuliko yote waliyopata kushambulia meli za kigeni.

NATO na majeshi ya kupambana na uharamia ya Umoja wa Ulaya wanasema maharamia walivamia meli hiyo kwenye bahari ya Hindi Jumatatu, kiasi cha kilomita 740 kaskazini-mashariki ya visiwa vya Ushelisheli. Ripoti zinasema maharamia wakiwa kwenye boti ndogo mbili, waliifuata meli hiyo na kuishambulia kwa risasi na makombora. Meli hiyo ilitumia mbinu za kiulinzi na kukimbia.

Hakuna majeruhi yeyote aliyeripotiwa. EU inasema ndege maalum zimepelekwa kuwatafuta maharamia hao. Wakati huo huo maafisa wa jeshi la majini walisema Jumatatu kuwa maharamia wa ki-Somali wameteka nyara meli moja ya mizigo iliyojaa silaha.

Taarifa kutoka shirika la habari la Reuters na orodha ya jarida la usafirishaji la Lloyd, inasema meli hiyo ilikuwa ikifanyakazi kwa kutumia jina bandia, Al Mizan. Hakuna yeyote kutoka maafisa wa ukaguzi wa majini au maafisa wa Somalia aliyethibitisha taarifa hiyo.

XS
SM
MD
LG