Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 26, 2023 Local time: 06:53

Miaka 20 baada ya kuanguka ukuta wa Berlin


Ukuta wa Berlin ulogawa mji mkuu huo na Ujerumani kati ya mashariki na magharibi ulijengwa miongo mitatu kabla ya kuanguka. Ulikua alama kuu kabisa ya vita vya baridi duniani. Lakini hatimae malalamiko na mapinduzi ya amani katika kanda hiyo yalipelekea kuporomoka na kuungana tena kwa Ujerumani, mwisho wa vita baridi na mabadiliko ya kisiasa huko Ulaya na kwengineko.

Kuwakilisha mlolongo wa matukio hayo, dhumna kubwa kabisa zimetengenezwa kuchorwa na kupangwa kwa umbali wa kilomita moja na nusu mahala ukuta ulikuwepo.

Meya wa berlin Klaus wowereit alizindua maonesho hayo Jumapili na alisema, “Dhumna hizi zimechorwa na vijana wa kijerumani lakini pia kutoka sehemu nyinginezo za dunia. Mradi huo unalengo la kuwasomesha kuhusiana na wakati huo katika historia na kuwahamasisha kuporomosha kuta na vizuizi kokote vinakopatikana”.

Katika kuadhimisha siku hiyo sherehe ni pamoja na tamasha za muziki hadharani, hotuba na zitahitimishwa kwa maonesho makubwa kabisa ya fashasa usiku wa Jumatatu.

Lakini kutokana na kuwepo kwa viongozi wa kisiasa na wageni wa heshima kutoka kila pembe ya dunia, itakua nafasi nzuri kwa mikutano ya kisiasa, mazungumzo na hotuba.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa marekani Hilary clinton anahudhuria sherehe hizo alizungumza Jumapili usiku katika dhifa iliyotayarishwa na Marekani kuadhimisha siku hiyo.

Akizungumza alisema “Tunajilipa sisi wenyewe na wale wote wanao tumaini kupata uhuru kama huo ambao unafurahiwa au hata kutotiliwa manani huko berlin hii leo. Na tunahitaji kubuni ushirikiano wenye nguvu zaidi kuporomosha kuta zilizopo katika karne ya 21”.

XS
SM
MD
LG