Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 21:15

Warepublican na Wademocratic watofautiana juu ya ushindi Marekani


Viongozi wa chama cha Republican na Democratic nchini Marekani wanatofautiana kufuatia uchaguzi wa baadhi ya majimbo Jumanne, ambapo wa-Republican walishinda kwenye majimbo mawili kati ya matatu yaliyofanya uchaguzi.

Mwenyekiti wa chama cha Republican, Michael Steel, anasema ushindi wa kweli wa matokeo ya upigaji kura siku ya Jumanne kwa wale wote ambao walichukua hatua dhidi ya kile alichokiita kuchoshwa na ajenda za serikali ya Washington. Kwenye mkutano na waandishi wa habari Jumatano, Steel alisema huu ni mwanzo mpya wa Republican.

Wagombea wa chama cha Republican walipata ushindi mkubwa kwenye majimbo ya Virginia na New Jersey. Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa walisema idadi ya kura katika majimbo mawili zinaonesha namna wapiga kura walivyohama kutoka Democratic na kuwaunga mkono wagombea wa Repuplican.

Wakati huo huo msemaji wa White House Robert Gibbs, alisema kinyang’anyiro cha kiti cha gavana kinaonesha kwamba wapiga kura walikwenda kwenye vituo vya kupigia kura kuwajibika na masuala ya ndani ya jimbo ambayo hayamuhusishi Rais Obama.

XS
SM
MD
LG