Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 08:47

Wakimbizi wa Congo warudi nyumbani


Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema zaidi ya wakimbizi mia tano wa DRC wamerudi nyumbani siku ya Jumatano kutoka Zambia, na kufanya idadi ya wakimbizi wanaorudi nyumbani kufikia zaidi ya elfu kumi na tano na mia sita tangu mwezi Mei.

Shirika hilo linasema kundi la hivi karibuni la wakimbizi liliondoka kaskazini mwa nchi ya Zambia kwa kutumia boti, kuelekea Moba na Kalemie huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mwakilishi wa shirika hilo nchini Zambia, James Lynch, alielezea zoezi la uondokaji huo kama mafanikio na aliwasihi zaidi wakimbizi wa Congo kurudi makwao.

Zambia hivi sasa inawahifadhi wakimbizi wa Congo 34, 671, wengi wao walikimbia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe muongo mmoja uliopita. Nusu ya wakimbizi hao wanaishi kwenye makambi. Takribani wa-Congo elfu kumi walirudi makwao kutoka Zambia mwaka 2008 na zaidi ya wakimbizi elfu saba mwanzoni mwa mwaka 2007.

XS
SM
MD
LG