Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 05:54

AU yajaribu kutanzua mzozo wa Madagascar


Rais wa sasa wa Madagascar Andry Rajoelina, alikaa upande mmoja wa ukumbi mkubwa wa Umoja wa Afrika. Nae rais aliyemng’oa madarakani mapema mwaka huu, Mark Ravalomana, alikaa upande wa pili wa ukumbi huo.
Hawakupeana mikono, wala hawakutowa hata ishara ya kutambua kuwepo kwa mwengine kwenye mkutano huo.

Marais wengine wawili wa zamani Didier Ratsiraka na Albert Zafy, pia walikuwemo katika ukumbi huo, kadhalika mwenyekiti wa kamisheni ya AU Jean Ping, ambaye aliwakumbusha kwamba madhara ya kiuchumi na ya kisaikologia yanawaathiri raia wa Madagascar, kwa kuchelewesha kwao kutatuwa mzozo huo wa kisiasa.

Amesema “Ukweli kama unavyo ujuwa, huko Madagascar, unatambulishwa na machofu ambayo watu wa Madagascar wanahisi, watu ambao wanataraji mzozo utamalizika. Mzozo ambao watu wote wamesozwa. Na hali ya kiuchumi na kijamii nchini kwenu inazidi kudumaa kila siku. Watu wa Madagascar wanastahiki maisha bora ya baadaye, na hilo linawategemea nyinyi.”

Bw. Ping aliwaambia vyama hivyo vinne,kwamba watahukumiwa vikali iwapo watakosa kufikia maelewano juu ya kuundwa kwa serikali ya mpito, ambayo itapelekea kuandaa uchaguzi mpya mwakani.

Lakini matamshi walotoa viongozi wanaohasimiana,kabla ya mkutano huo kuanza, yanaonesha majadiliano yanakabiliwa na changemoto kubwa.
Bw. Rajoelina alinukuliwa akisema kabla ya kuondoka Antananarivo,kwamba yeye hatotoa ridha zaidi ya alizotowa wakati wa mikutano ya awali yalofanyika huko Msumbiji.

Nae Bw. Ravolamana alisaema hapo mapema kwamba yeye hatokubali kushiriki kwenye majadiliano hadi pale Rajoelina, ameondoka kwanza kutoka madarakani.

XS
SM
MD
LG