Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 15:07

Wako Apigwa Marufuku Marekani


Mkuu wa Sheria nchini Kenya Amos Wako, ni miongoni mwa maafisa waandamizi wa nchi hiyo waliozuiwa kuingia marekani.Balozi wa marekani nchini Kenya, Michael Ranneberger alimtaja Wako kwa njia ya Twitter kwenye mtandao wa mawasiliano jumapili.

Marekani ilitangaza wiki iliyopita kuwa imefuta visa ya afisa mkuu wa Kenya ambaye ilimtuhumu kwa kuzuia mabadiliko ya kisiasa. Balozi aliuliza watumiaji wa mtandao wa Twitter jumapili ikiwa wanashangaa ni afisa gani wa Kenya aliyezuiwa kuingia marekani.

Baadaye alitoa jibu na habari kwa gazeti la Kenya la The standard lililomtaja Wako kama afisa aliyezuiwa. Ranneberger amekuwa akitumia Twitter kwenye mtandao wa mawasiliano mara kadhaa katika miezi miwili iliyopita kujibu maswali kuhusu maendeleo ya kisiasa nchini Kenya.

XS
SM
MD
LG