Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 18:17

Habari kuu Kenya na Marekani wiki hii


Nchini Kenya shinikizo la Marekani la kutaka mabadiliko ya haraka ya kisiasa limezua mtafaruku baina ya taifa hilo la Afrika Mashariki na Marekani. Naibu Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Johnnie Carson wiki hii alitangaza kupigwa marufuku kwa afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Kenya kuingia nchini Marekani.

Bwana Carson aliashiria kuwa afisa huyo ni kikwazo kikubwa kwa mabadiliko ya kisiasa nchini humo. Akizungumza na sauti ya Amerika, mwandishi habari wa gazeti la Daily Nation Douglas Mutua, alisema tishio la waziri wa mambo ya nje wa Kenya bwana Moses Wetangula kuwa Kenya italipiza kisasi tangazo hilo la Marekani ni kama mzaha mkubwa, kwani Kenya inaihitaji Marekani kuliko Marekani inavyoihitaji Kenya.

Bwana Mutua alisema Marekani inaijali Kenya na haitaki kuona ikitumbukia tena katika ghasia za kisiasa wakati wa uchaguzi ujao wa mwaka 2012. Bwana Carson alisema mabadiliko hayo yatanusuru Kenya kuingia katika machafuko mengine ya kisiasa, athari ambazo huenda zikadhuru nchi jirani na hata ukanda wa maziwa makuu.

Akizungumza katika Meza ya waandishi habari pia, mwandishi wa habari wa Atlanta, Georgia BMJ Mureithi, alisema utawala wa rais Barack Obama unakabiliwa na changamoto kubwa kuhusiana na swala la kuongeza majeshi ya Marekani nchini Afghanistan. Bwana Mureithi alisema Marekani imepata pigo kubwa wiki hii baada ya wanajeshi wake 18 kuuwa nchini humo, huku ghasia zikionekana kuongezeka nchini humo. Mureithi pia alisema mkutano baina ya wajumbe wa nchi za Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara uliodahminiwa na Marekani mjini Atlanta, unatazamiwa kuboresha uhusiano wa kibiashara baina ya Marekani na nchi hizo, kwa kuimarisha uchukuzi wa safari za ndege baina ya bara hilo na Marekani.

XS
SM
MD
LG