Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 06:38

Msumbiji wapiga kura kwa amani


Watu walianza kusimama kwa foleni tangu alfajiri, hata kabla ya vituo vya kupiga kura kufunguliwa kote nchini humo siku ya Jumatano ili kupiga kura mapema kuchagua serekali mpya na wabunge wapya.

Rais Armando Guebuza wa chama tawala cha Frelimo alikua miongoni mwa watu wa kwanza kupiga kura mjini Maputo. Anagombania kwa mhula wa pili wa miaka mitano.
Alitoa mwito kwa raia wote wa Msumbiji kupiga kura kwa hali ya furaha bila ya ghasia.

Mwanasiasa mkongwe Afonso Dhlakama wa chama cha RENAMO, pia alipiga kura mapema. Wakati wa kampeni alilalamika dhidi ya kuwepo kasoro chungu nzima.

Alisema suala kuu ni kwamba, lazima uchaguzi uwe wa huru na wa haki. “Hiyo ni njia pekee anaeshindwa kuweza kukubali matokeo na mshindi kuweza kutawala kwa haki”.

Kampeni za mwaka huu zilipata nguvu kutokana na kuwepo na mgombea mpya wa tatu wa chama kipya cha Mozambique Democratic Movement kinachongozwa na Daviz Simango, ambae ni meya wa mji wa Beira, mji wa pili kwa ukubwa nchini Msumbiji. Simango mwenye umri wa miaka 45, alikua mwanachama wa chama kikuu cha upinzani cha RENAMO.

Bi Maria Armaida, mkazi wa Beira anasema kwa wakati huu hana hakika nani atapata ushindi katika bunge, kwani anasema wakati wa kampeni kila chama kiliweza kuwavutia watu wengi sana kwenye mikutano yao, hivyo haijulikani wapiga kura wanampendelea nani zaidi.

Wachambuzi wanamini chama cha FRELIMO kitarudishwa madarakani na Rais Guebuza atapata ushindi kwa mhula wa pili.

XS
SM
MD
LG