Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 18:20

Burundi inawatia kizuzini mabalozi wake wawili


Mabalaozi wawili wa Burundi, yule anaeiwakilisha nchi mjini Nairobi, Kenya, na yule wa Rome, Italy, walikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbiura walipowasili, kwa tuhuma za wizi wa maelfu ya dola zilizotolewa kwa ajili ya matumizi ya ofisi za balozi hizo.

Serekali ya Burundi hapo mwanzoni iliwaita nyumbani mabalozi hao, lakini maafisa wa usalama waliwakamata walipowasili na kuwaweka kizuizini mara moja. Hatua hiyo imewakera watu wengi na wapinzani nchini kwa vile mabalozi hao walikua maafisa wa vyeo vya juu wa serekali na hawakupewa kinga za za kibalozi au haki ya kufikishwa mahakamani.

Pancrase Cimpaye msemaji wa chama cha Fredebu alizungumza na Sauti ya Amerika na kusema kuwa hatua iliyochukuliwa na serikali ina ushawishi wa kisiasa na wala haihusiana na suala la wizi wa fedha.

Anasema ikiwa ilihusiana na ulaji rushwa basi huko huko Bujumbura kuna watu wengi wanaopora mamilioni ya dola na kuachiwa huru ukilinganisha na fedha zinazodaiwa kuchukuliwa na mabalozi hao ambazo amesema ni kidogo mno.

Bw Chimpaye ameongeza kusema kuwa upinzani haungi mkono hatua hiyo kwa vile ni kinyume cha sheria na haikufuata taratibu za mahakama. Anasema huwenda inatokana na mvutano wa ndani wa chama ambapo wanachama wengi hawaridhiki na uwongoizi wa chama.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG