Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 15:39

Marekani inamnyima afisa wa juu Kenya visa


Naibu waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, anaeshughulikia masuala ya Afrika Johnnie Carson, amekua na mikutano mjini Nairobi siku ya Jumatatu na maafisa wa vyeo vya juu ya masuala muhimu ya mageuzi serekali ya Kenya inahitaji kutekeleza.

Baada ya mikutano hiyo akizungumza na waandishi habari huko Nairobi, alitangaza marufuku ya kusafiri dhidi ya afisa wa juu mwenye ushawishi ambae hakutajwa kwa kuzuia mageuzi muhimu ya serekali.

Mwezi moja iliyopita Carson aliwapelekea barua maafisa 15 wa Kenya akiwatishia hatua kuchukuliwa ikiwa hawataanza kutekeleza mageuzi ya serekali. Balozi wa Marekani nchini Kenya Michael Ranneberger, alikua ametangazakwamba baadhi ya walopelekewa barua watazuiliwa hivi karibuni kusafiri hadi Marekani.

Wakuu wa serekali walitoa ahadi kwa miezi sasa alisema naibu waziri, akiongezea kwamba Marekani itaendelea kuhimiza maendeleo yafanyike katika suala la mageuzi.

"Msimamo wa Rais Obama ni Wazi. Tutaendelea kushikilia na kuongeza kishinikizo hatua kwa hatua kwa ajili ya utekelezaji na mambo hayatakua ya kawaida na wale wanaopinga mageuzi au walounga mkono ghasia" alisema Bw Carson.

Mpango wa mageuzi ulikua msingi wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Rais Mwai KIbaki na waziri mkuu Raila Odinga, baada ya Bw Kibaki kutangazwa kwa njia ya utata mshindi wa uchaguzi ulokua na ugomvi wa Disemba 2007.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG