Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:09

Mkataba mpya wa waliopoteza makazi Afrika


Mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Kampala umeidhinisha mkataba wa kwanza wa kipekee wa haki za waliopoteza makazi yao ndani ya nchi IDP's. Lakini mkutano huo haukupata uungaji mkono mkubwa wa nchi wanachama kutokana na kutohudhuria viongozi wengi walioalikwa kwenye mkutano huo.

Mkataba wa Kampala wa haki za waliopoteza makazi yao ulitiwa saini siku ya Ijumaa, katika sherehe kuu nje ya mji wa Kampala katika hoteli ya kifahari.

Rais wa Zambia Rupiah Banda alikua miongoni mwa viongozi wa kwanza kuidhinisha mkataba huo. Aliueleza kuwa mafanikio makubwa baada ya miaka kadhaa ya kazi nyingi za kutafuta muafaka.

Alisema, "nina amini ninazungumza kwa niaba ya wote wanaohudhuria mkutano huu ninaposema mkutano ulikua wa mafanikio maalum."

Wakuu wa mashirika mengi ya huduma za dharura walishuhudia kutiwa saini mkataba huo. Kamishna mkuu wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, alisema, "mkataba ni wajibu wetu kuulinda. Na ninatoa mwito kwa sehemu nyingine za dunia kuidhinisha mkataba muhimu kama huu, ikiwa ni chombo cha kuwalinda waliopoteza makazi yao."

Mkataba huo kwa mara ya kwanza unalazimisha wote Mataifa ya Kiafrika na makundi ya waasi yenye silaha kuzuia kuwafurusha watu kutoka makazi yao na kuwapatia haki za kimsingi wale waliofukuzwa kutoka kwenye makazi yao kutokana na vita na maafa ya kimaumbile.

XS
SM
MD
LG