Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:52

Afrika kusaini makubaliano kuwalinda wakimbizi


Nchi 46 za bara la Afrika zinatarajiwa kutia saini makubaliano leo Ijumaa, kuwalinda na kusaidia watu waliotoroshwa manyumbani mwao kutokana na ghasia.

Maafisa kutoka nchi hizo za Afrika wanakutana katika mji wa Uganda, Kampala, kumalizia maelezo ya kina juu ya mswada mpya, ambao unatilia mkazo haki za raia katika maeneo yenye mgogoro. Maafisa hao wanasema hati hizo zinaweka wazi mswada halali ambapo serikali na makundi ya waasi wenye silaha yanatakiwa kuwalinda na kuwasaidia raia wa kawaida kutokana na vita.

Kuna wakimbizi takribani milioni 17 na watu waliolazimika kutoroka makwao ndani ya nchi zao, katika bara la Afrika. Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya wakimbizi Antonio Gueterres, alizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo Alhamisi, akiziomba serikali za Afrika kuwajibika kwa wakimbizi hao.

Kamishna huyo wa Umoja wa Mataifa alieleza kuwa idadi ya wakimbizi katika bara la Afrika imeshuka na kufikia watu milioni 2.3, lakini alisema hii imetokana na kuongezeka haraka kwa idadi ya watu walifurushwa makwao ndani ya nchi zao kutokana na migogoro, ukame na matatizo mengine ya kijamii.

XS
SM
MD
LG