Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:30

Guinea kupelelezwa kwa kukiuka Haki za Binadamu


Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linaunga mkono kubuniwa kwa tume huru ya kupeleleza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Guinea mwezi uliopita, wakati maandamano ya kupinga serikali yalipogeuka kuwa maafa makubwa.

Makundi ya haki za kibinadam na mashahidi wanasema kwamba wakati wa maandamano ya September 28 katika uwanja wa michezo katika mji mkuu Conakry, waandamanaji walifyatuliwa risasi, kukatwa kwa visu, kubakwa na kupigwa.

Wanasema takriban watu 157 waliuwawa, idadi ambayo serikali inapinga na kusema ni juu sana.

Wiki ilopita katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, alitangaza kuwa ataanzisha tume ya kimataifa ya upelelezi, ili kuchunguza visa hivyo na wale walohusika wawajibike. Anasema amempeleka mmoja wa maafisa wake wakubwa. Naibu katibu wa masuala ya kisiasa Haile Menkarios huko Conakry, kwenda kuanzisha tume hiyo.

Bwana Menkarios aliripoti matokeo yake kwa baraza la usalama katika mkutano wa siri. Baadaye, aliwaambia waandishi wa habari kwamba kiongozi wa kijeshi wa Guinea Moussa Camara, amekubali kushirikiana na tume hiyo ikishabuniwa.

XS
SM
MD
LG