Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 10:08

Kibaki awaahidi wakenya katiba mpya


Sherehe za mwaka huu za kuadhimisha mwaka wa 46 wa siku ya Kenyatta Day ziligubikwa na majonzi makubwa baada ya jengo la ghorofa tatu kuanguka ghafla katika mji wa Kiambuu katika viunga vya mji mkuu wa Nairobi, wakati wafanyakazi katika jengo hilo wakiendelea na ujenzi.

Licha ya maafa hayo mamia ya watu walifurika katika uwanja wa Nyayo mjini Nairobi katika sherehe za kuwakumbuka wapigania uhuru wa Kenya, pamoja na muasisi wa taifa hilo, marehemu Mzee Jomo Kenyatta.

Hotuba ya Rais Mwai Kibaki kwenye sherehe hizo iligusia zaidi suala nyeti la marekebisho ya katiba akasema kwamba juhudi zinafanywa na serikali ili kuhakikisha kwamba katiba mpya inapatikana mwaka ujao.

Vile vile makamu wa Rais nchini humo bwana Kalonzo Musyoka aligusia suala hilo hilo la mageuzi ya katiba, akisema ana hakika katiba mpya itandikwa. Waziri mkuu wa Kenya bwana Raila Odinga hakuhudhuria sherehe kwa sababu yuko ziarani China.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG