Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 07:51

Al Shabab wadai kutungua ndege ya Marekani


Kundi la waasi la al-Shabab nchini Somalia linasema wapiganaji wake wameitungua ndege moja ya upelelezi ya Marekani.

Msemaji wa al-Shabab aliambia Sauti ya Amerika kuwa ndege hiyo isiyokuwa na rubani ilitunguliwa Jumatatu na kuanguka baharini karibu na mji wa bandari ya Kismayo. Msemaji huyo anasema ndege hiyo ilikuwa angani kusini mwa mji wa Somalia kwa siku kadhaa.

Anasema kundi hilo la al-Shabab linatafuta mabaki ya ndege hiyo. Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa juu ya madai hayo. Marekani imetumia ndege zinazosafiri bila marubani katika miaka ya hivi karibuni, kuwatafuta wababe wa kivita wa Somalia, maharamia na washukiwa wa ugaidi.

XS
SM
MD
LG