Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:29

MDC yaacha kujihusisha na serikali ya Umoja ya Zimbabwe


Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amesema Ijumaa anaacha kujishirikisha na chama tawala cha ZANU-PF cha Rais Robert Mugabe, lakini hajajitoa rasmi kutoka kwenye serikali ya kushirikiana madaraka.

Bwana Tsvangirai alisema Ijumaa kuwa chama chake cha Movement for Democratic Change-MDC hakitahudhuria mikutano ya baraza la mawaziri au kujihusisha na kazi za kiutendaji na chama cha ZANU-PF, ambacho alikiita hakiko wazi na mshirika asiyetabirika.

Alisema chama cha MDC kitaendelea kufanya kazi zake za bunge. Kujitoa kwa chama hicho kunafuatia kukamatwa kwa mwanachama mwandamizi wa chama cha MDC Roy Bennett, ambaye aliteuliwa na chama chake kuwa naibu waziri wa kilimo.

Bennett alikamatwa wiki hii kufuatia kesi ya shutuma za ugaidi. Aliachiwa huru kwa dhamana siku ya Ijumaa. Bwana Tsvangirai anasema kukamatwa kwa Bennett ni ushahidi kuwa chama cha ZANU-PF kinakitazama chama cha MDC kama mshirika wa mbali.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Robert Wood, siku ya Alhamisi aliuita ukamataji wa Bennett kama jaribio la dhahiri kumzuia asiweze kufanya kazi yake. Bennett anashutumiwa kuwa na silaha kinyume cha sheria ili kuipindua serikali ya Mugabe, na mwanzoni mwa mwaka huu alikaa jela kwa muda wa mwezi mmoja kwa shutuma hizo hizo.

XS
SM
MD
LG