Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:51

Marekani yaionya Zimbabwe kutokana na mivutano ya kisiasa


Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema mashtaka ya ugaidi dhidi ya mbunge wa Zimbabwe Roy Bennet ni ukosefu mkubwa wa kisheria katika nchi hiyo ya Afrika.

Marekani pia inasema ni msaada wa kibinadamu pekee utakaotolewa kwa Zimbabwe, hadi serikali ya rais Mugabe itakapo kubali mabadiliko ya muafaka wa kushirikiana madaraka.

Utawala wa Obama unayashutumu mashtaka dhidi ya Roy Bennet kwa maneno makali, ukisema bayana kuwa hautoiga mfano wa Uingereza na kutowa msaada mpya kwa serikali ya muungano inayoongozwa na rais Mugabe.

Bennet ambaye ni mwanachama mwanzilishi na vilevile mweka hazina wa chama cha Movement for Democratic Change, katika serikali ya muungano alifungwa hiyo alhamis na kuamrishwa kufikishwa mahakamani kwa mashtaka ya awali ya kuwa na silaha za kigaidi kitisho kwa serikali ya Mugabe.

Chama cha MDC kinachoongozwa na waziri mkuu Morgan Tsangirai kinasisitiza kuwa Bw. Bennet hakutenda makosa kikisema kufungwa kwake ni tishio la kusudi la wafuasi wa chama cha Bw. Mugabe Zanu PF.

XS
SM
MD
LG