Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 06, 2023 Local time: 07:01

Mahakama yaidhinisha ushindi wa Ali Ben Bongo


Mahakama ya katiba ilihesabu upya kura kutoka vituo 2,800 na imethibitisha ushindi wa kijana wa rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar Bongo.

Akitangaza matokeo hayo kwenye televisheni ya taifa rais wa mahakama ya katiba Marie Madeleine Mborantsuo alisema mahakama ilifutilia mbali matokeo kutoka kituo kimoja cha uchaguzi, lakini kutokana na kura nyingi alizopata bw Bongo dhidi ya wapinzani wake, alisema uchaguzi wake kama rais wa Jamhuri ya Gabon umethibitishwa.

Uwamuzi wa mahakama ni wa mwisho na unafungua sasa njia ya kuapishwa kwa rais mteule. Uamuzi huo unafutilia mbali madai yaliyofikishwa na waziri wa zamani wa mambo ya ndani Andre Mba Obame na kiongozi wa upinzani Pierre Mamboundou. Kila moja kati yao alijipatia asilimia 25 ya kura wakati Bw Bongo alijipatia asilimia 42.

Wakati Bw Bongo alipotangazwa mshindi hapo mwezi Agosti, polisi walipambana na waandamanaji wa upinzani katika mji mkuu, na inaripotiwa watu watatu waliuawa katika ghasia hizo.

XS
SM
MD
LG