Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 12:44

HRW yaishutumu DRC kutowajali raia wake


Kundi la Human Rights Watch-HRW linasema oparesheni za kijeshi za serikali ya Congo huko mashariki mwa Congo haziwasaidii wananchi wake. Akizungumza kwa niaba ya umoja wa wanasheria wa Congo, HRW inawasihi wanadiplomasia na maafisa wa Umoja wa Mataifa kuzungumzia namna ya kuwalinda wananchi wa eneo la mashariki mwa Congo baadae wiki hii wakati wanapokutana mjini Washington, DC.

HRW inasema zaidi ya wa-Congo 1,000 wameuwawa, wanawake 7,000 wamebakwa na zaidi ya nyumba 6,000 zimechomwa moto huko mashariki katika majimbo ya Kivu Kusini na Kaskazini tangu mwezi Januari mwaka 2009.

Umoja huo unasema mauaji mengi yanafanywa na kundi la uasi la kihutu kutoka Rwanda, lijulikanalo kama Democratic Forces for the Liberation of Rwanda-FDLR.

Umoja wa wanasheria wa Congo ulianzishwa mwezi Julai mwaka 2008 kwa lengo la kuangalia mvutano uliopo juu ya kuwalinda wananchi na kuheshimu haki za binadamu kama sehemu ya hatua za amani huko mashariki mwa Congo.

XS
SM
MD
LG