Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 23:17

Polisi Burundi wazuia wakimbizi wa DRC kurudi kwao


Polisi wa Burundi wamewazuia wakimbizi wapatao 2,000 kuondoka kwenye kambi na kurudi kwenye nyumba zao huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Katika muda wa siku tatu zilizopita wakimbizi wamejazana katika barabara na polisi walifyatua risasi baada ya kufunga kambi ya Gihinga katika mpango wa kuwahamishia wakimbizi hao kwenye kambi nyingine karibu na mpaka wa Tanzania. Wakimbizi hao waligoma kuhama na kuanza juhudi za kuondoka kwenda Congo kwa kutumia njia ya miguu.

Wakimbizi hao waliombwa na shirika husika kuendelea kukaa Burundi kwasababu ya mapigano yanayoendelea na ghasia katika jimbo la Kivu kusini huko DRC.

Sauti ya Amerika imezungumza na Kieri Musole,mkurugenzi wa shirika la ndani la kuhudumia wakimbizi nchini Congo,liitwalo Msaada na Pendo la Amani.

XS
SM
MD
LG