Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:31

Habari kuu za wiki Kenya na Tanzania


Wiki hii misukosuko ya kisiasa ilitawala nchi mbili za Afrika Mashariki Kenya na Tanzania. Mhariri wa gazeti la Mwananchi Salim Said aliyeleza kuwa kwa mara ya kwanza viongozi mashuhuri na wenye ushawishi wa kisiasa akiwemo katibu mkuu wa zamani wa umoja wa Afrika Dr. Salim Ahmed Salim amewaambia wanachama wa chama tawala CCM kuwa na wao pia wako huru kujitosa katika uwanja kugombania urais mwaka ujao.

Kauli yake hiyo ilishangaza wengi kwani kuna baadhi ya wanasiasa wanaomtaka Rais Jakaya Kikwete abaki kama mgombea urais pekee wa chama hicho. Akijibu kauli hiyo ya Katibu mkuu, Katibu mkuu wa chama hicho cha CCM bwana Yusuf Makamba alisema Tanzania inazingatia demokrasia na kwamba hata bwana Salim ana haki ya kugombea kiti hicho akipenda.

Na kutoka Kenya, mtangazaji wa radio na Televisheni ya Citizen Franklin Wambugu aliiambia meza ya waandishi habari kuwa Kujiuzulu wiki hii kwa jaji Aaron Ringera kulitokana na shinikizo kali kutoka kwa bunge, makundi ya kutetea haki za kiraia na jumuiya ya kimataifa. Bwana Wambugu pia alizungumzia ziara ya wiki ijayo ya katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Koffi Annan nchini humo pamoja na mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ICC Louis Moreno Ocampo.

Ocampo anakwenda Kenya baada ya waziri wa sheria Mutula Kilonzo kumweleza kuwa Kenya imeshindwa kubuni mahakama maalum kusikiliza kesi za wachochezi wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007, na kwa hiyo yuko huru kuwachukulia hatua watuhumiwa hao.

XS
SM
MD
LG