Rais Mwai Kibaki wa Kenya alimteua tena mkuu aliyekua na utata kuiongoza Tume ya kupambana na ulaji rushwa, Aaron Ringera na kuzusha malalamiko makubwa kote nchini na kubaki kwenye vichwa vya maneno vya vyombo vya habari kwa wiki kadhaa.
waandamanaji wakidai uchunguzi dhidi ya Ringera (Sep 2006) |
Ringera mwenyewe siku ya Jumatano alimaliza mivutano hiyo kwa kuamua hatimae kujiuzulu baada ya kudaia kwa ukaidi wiki iliyopita kwamba hatoacha nafasi hiyo. Alisema, "naibu mkurugenzi Fatouma Sichake na mimi binafsi tulifikia uwamuzi kutokana na yote yanayotokea kwamba itakua kwa masilahi ya Kenya, Kamisheni ya ulaji rushwa ya Kenay kama taasisi na wafanyakazi wake wote kwangu mimi kuijiondoa kutoka uwongozi wa kamisheni hiii."
Wiki mbili zilizopita bunge lilipinga kuidhinisha kuteuliwa kwake baada ya majadiliano makali ya siku kadhaa ni mivutano ya kisiasa katikavikao vya faragha. Rais alikata kutambua kura ya bunge, akishikilia kwamba uteuzi ni chini ya mamlaka yake na kwamba ni mahakama ya taifa ndiyo inayoweza kuchukua uwamuzi.