Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 09:41

Jumuia ya kimataifa yalani mauwaji ya Guinea


Kiongozi wa kijeshi wa Giuinea Kapteni Moussa Guinea Kapiteni MoussaDadis Camara anajaribu kujitenga na mauwaji ya karibu watu 150 yaliyotokea baada ya vikosi vya usalama kupambana na waandamanaji katika mji mkuu wa Conakry.

Idadi ya walofariki haijulikani wazi kutokana na ripoti kwamba polisi wa majeshi wamekuwa wakikusanya maiti wenyewe badala ya kuyawachia makundi ya haki za binadamu kuhesabu idadi ya walouliwa.

Mapema wiki hii wanadamanaji walikusanyika katika uwanja mkuu wa mpira wa Conakry kulalamika uwezekano wa Kapteni Camara kugombania kiti cha rais wakati wa uchaguzi mkuu ulopangwa kufanyika baadae mwaka ujao.

Akijaribu kujitenga na mauwaji hayo ya Jumatatu ambapo vikosi vya usalama vinasemekana vilifyetua risasi dhidi ya waandamanaji, Kapteni Camara ameiambia kituo kimoja cha redio cha Senegal RFM kua alitaka kutembelea eneo lililozuka ghasia, lakini alishauriwa na maafisa wake wa usalama kwamba hali si ya usalama.

Alisisitiza kwamba hataki kuona ghasia zinatokea kwani hakuchukua madaraka ili kupambana na wananchi wa Guinea. Kiongozi huyo alichukua madaraka kutokana na mapinduzi yasiyo mwaga damu mwezi Disemba mwaka jana, na ameahidi kuitisha uchaguzi wa huru na haki.

Makundi ya kutetea haki za binadam zinamtaka Kapteni Camara kuamrisha uchunguzi mara moja ikiwa kweli hakukusika na ghasia hizo. Mtafiti wa Human Rights Watch huko Afrika Magharibi Corinne Dufka anasema, "kwa Dadis Camara kudai kwamba vitendo vilifanywa na baadhiu ya wanajeshi walokua na hasira , ni jambo lisilokubalika kamwe. Hii ianonekana ilikua operesheni iliyopangwa vyema. Ikiwa ana nia ya dhati basi inabidi aamrishe uchunguzi mara moja na kuchukua hatua thabiti za kuwawajibisha ewalohusika na vitendo hivyo."

XS
SM
MD
LG