Rais wa Marekani Barack Obama anasema Marekani haiwezi kumaliza matatizo ya dunia peke yake na imetoa wito wa enzi mpya ya mahusiano duniani kote.
Kiongozi huyu wa Marekani alitoa rai hiyo wakati wa hotuba yake katika baraza kuu la umoja wa mataifa ambalo limeanza New York Jumatano.
Bw.Obama aliahidi kufanya kazi kwa uwazi na kwa haki na ustawi nyumbani na nje ya nchi. Lakini aliongeza lazima mataifa yote yawajibike kwa kutoa majibu ya kimataifa ili kupambana na matatizo ya kidunia, ikiwa ni pamoja na umaskini na mabadiliko ya hali ya hewa, uchumi na kuzuia usambazaji wa nyuklia.