Rais Barack Obama amesema Marekani imenuwia kuchukua hatua katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuonya kutochukuliwa hatua kimataifa kunaweza kupelekea maafa yasiyoweza kubadilishwa tena.
Bw Obama aliwahimiza zaidi ya viongozi 90 wa dunia wanaokutana mjini New York, kwa mkutano wa viongozi juu ya mabadiliko ya hali ya hewa, kufanya kazi pamoja kupambana na tatizo hilo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki -moon aliyetayarisha mkutano huo, aliufungua siku ya Jumanne akisema itakua jambo lisiloweza kua na msamaha ikiwa hawatachukua hatua.
Marekani na China zinaangalia namna ya kufufua mazungumzo yaliyokwama juu ya mabadiliko ya hali ya hewa leo Jumanne, wakati viongozi wa dunia wanakutana New York kwa ajili mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Maafisa wanamatumiani kufanya maendeleo kufikia mkataba wa kimataifa wa hali ya hewa ambao serekali za dunia zina mpango wa kuidhinisha wakati wa mkutano wa Copenhegan huko Denmark mwezi wa disemba.
Bwana Obama anasema utawala wake unachukua hatua za haraka kupambana na juhudi mpya za mabadiliko ya hali ya hewa, lakini hajaweka bayana ni haraka ya kiasi gani wabunge wa Marekani wanajizatiti kukabiliana na uchafuzi wa hewa chafu.