Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 18:32

Tume ya haki za binadamu Kenya yaenda Hague


Juhudi za kutetea haki za waathirika wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu uliopita nchini Kenya zinaendelea. Wiki iliyopita wajumbe wa mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali, pamoja na tume ya kitaifa ya haki za binadamu nchini humo walikutana na mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya The Hague nchini Uholanzi.

Akizungumza na Sauti ya Amerika, makamu rais wa tume ya haki za binadamu nchini Kenya, Hassan Omar, alisema kiini cha mkutano wao na bwana Luis Moreno Ocampo kilikuwa kumtaka mwendesha mashtaka huyo ajihusishe zaidi na suala hilo ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Bwana Omar alisema tume yake imevunjwa moyo na uzembe unaodhihirika katika baraza la mawaziri wa Kenya, la kuonesha kutojali katika kuwahakikishia wa-Kenya kuwa haki itatendeka.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG