Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 20:58

Wapinzani Gabon wapinga matokeo ya Bongo


Mahakama ya katiba ya Gabon inatafakari changamoto ya kisheria kuhusiana na uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita. Wapinzani wa Rais mteule Ali Ben Bongo wanataka ushindi wake ubatilishwe kwa sababu ya kile wanachosema uligubikwa na wizi mkubwa wa kura.

Wagombea wanne kati ya 17 ambao wanampinga rais mteule Bongo wanaitaka mahakama ya katiba ya Gabon kubatilisha uchaguzi wake kwa sababu wanasema matokeo kutoka zaidi ya theluthi mbili ya vituo vya kupigia kura yaliathiriwa na wizi wa kura uliofanywa na maafisa wa uchaguzi ili kumfaidisha Bongo. Wanasiasa hao walifungua mashtaka kabla ya tarehe ya mwisho ya kufanya hivyo.

Bwana Bongo ni mtoto wa kiume wa mtawala wa muda mrefu nchini Gabon, Omar Bongo,ambaye alikufa mwezi Juni baada ya kuwepo madarakani kwa miaka 42. Kifo chake kilitoa mwangaza wa kuwepomabadiliko nchini humo, japokuwa mtoto wake wa kiume ambaye alikuwa waziri wa ulinzi alitarajiwa kurithi nafasi ya baba yake.

Kutangazwa kwa ushindi wa chama tawala kulizusha ghasia za waandamanaji katika mji wa Port Gentil, ambapo waandamanaji wa upinzani walichoma ubalozi wa Ufaransa na walivamia ofisi za makampuni ya mafuta za Ufaransa na Marekani.

XS
SM
MD
LG